Nenda kwa yaliyomo

Bahari ya Java

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Bahari ya Java
Pwani ya Java Sea karibu na Anyer .

Bahari ya Java ni sehemu ya bahari iliyopo kati ya visiwa vya Indonesia vya Borneo kaskazini, Java upande wa kusini; Sumatra magharibi, na Sulawesi mashariki. Mlangobahari wa Karimata upo kwenye kaskazini magharini na kuiunganisha na Bahari ya Kusini ya China .

Eneo lake ni km² 320,000.

Uvuvi ni shughuli muhimu ya kiuchumi katika Bahari ya Java. Kuna zaidi ya spishi 3,000 za viumbe vya baharini katika eneo hilo. Kuna pia hifadhi kadhaa za kitaifa kama Karimunjawa.

Eneo linalozunguka Bahari ya Java ni shabaha maarufu ya utalii . Wengi wanakuja kupiga mbizi na kupata picha za viumbe chini ya maji, mabaki ya meli zilizozama, matumbawe na sifongo.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilitokea hapa mapigano ya baharini katika miezi ya Februari na Machi ya 1942 ambako jeshi la maji la Japani lilishinda mataifa ya ushirikiano Uholanzi, Uingereza, Australia na Marekani yaliyojaribu kutetea Java.

    Tovuti zingine

    Wikimedia Commons ina media kuhusu:

    5°S 110°E / 5°S 110°E / -5; 110