Nenda kwa yaliyomo

QR code

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 08:30, 28 Oktoba 2017 na Ndesanjo (majadiliano | michango)
Mfano wa QR code

QR code (Msimbo wa QR) (kutokana na Kiingereza Quick Response Code) ni maandishi au picha zilizo kwa mpangilio maalum ambazo huweza kusomeka kwa kutumia kifaa maalum kama simu janja (smartphone) ambayo huweza kutumia kamera kusoma hayo maandishi au picha ili kuweza kutambua data zilizoko ndani msimbo upau (barcode).


Teknolojia hii iliundwa huko Japani kwa ajili ya sekta ya magari ingawa hivi sasa inatumika katika sekta nyingine pia. Teknolojia hii ilipata maarufu nje ya sekta ya magari kutokana na usomaji wake wa haraka na uwezo mkubwa wa kuhifadhi data ikilinganishwa na msimbo upau wa UPC. Mambo ambayo teknolojia hii inaweza kuyashughulikia ni pamoja na kufuatilia bidhaa, kitambulisho cha bidhaa, kufuatilia wakati, nyaraka, n.k.

Msimbo huu huwa na miraba miyeusi iliyopangwa kwa mraba fito na rangi nyeupe nyuma yake ambayo inaweza kusomwa na kifaa kama kamera.

Viungo vya Nje